Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Masoud Ali Mohammed Akizungumza na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad alipokwenda kujitambulisha Ofisini kwake Vuga.
Mhe. Masoud amesema suala la ulinzi wa raia na mali zao ni jambo muhimu ambalo litawaongezea imani wananchi kutoa ushirikano kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Nae Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar amependekeza kuandaliwa kwa mafunzo ya pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Vikosi vya Idara Maalum ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wapiganaji hao. Kamishna Hamad Khamis Hamad amefika Ofisini hapo ujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni
Kwahabari zaidi usiache kutembelea Youtube Channel yetu OR-TMSMIM ZANZIBAR na kusubscribe
|
|
|
|