HUDUMA ZINAZOTOLEWA
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ina majukumu makuu yafuatayo:-
- Kusimamia Sera, Sheria na Kanuni mbali mbali za Ofisi.
- Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
- Kudumisha Amani, Ulinzi na Usalama katika Mikoa na Wilaya hadi Shehia.
- Kulinda mali za Taifa na za watu binafsi zisiharibiwe, kuzuia uingizaji au utoaji nje ya nchi kimagendo, pamoja na kusimamia kazi za uzimaji moto na uokozi.
- Kuwasajili na kuwapa vitambulisho Wazanzibari wakaazi.
- Kuwahifadhi kwa kufuata taratibu bora na kwa kuzingatia haki za binaadamu watuhumiwa na waliofungwa ambao wako katika Vyuo vya Mafunzo.
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya kuijengea uwezo Mikoa kitaaluma na utumishi katika Mikoa.
- Kutoa mwongozo na ushauri kwa Mikoa katika mambo ya kisheria na utaratibu, kujenga mazingira mazuri katika kuimarisha huduma za kijamii na kiuchumi katika Mikoa.
- Kuratibu, kushauri, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuliza Serikali za Mitaa.
- Kuimarisha Utawala Bora na kuimarisha uwezo wa Serikali za Mitaa na mamlaka zake.
- Kufuatilia na kukagua utendaji wa mamlaka za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika utoaji wa huduma.
- Kuendeleza michezo katika Idara na Taasisi zetu.
- Kuimarisha uhusiano baina ya taasisi za Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ. Na taasisi nyengine.