• MAONESHO YA NANE NANENibu Waziri Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar MHE Hasaan Khamis Hafidh akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea bandani hapo.
  • MAONESHO YA NANE NANEMaafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa Serikali Za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakitoa Elimu kwa Wanafunzi mbali mbali waliotembelea banda hilo.
  • UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MWAKA JKUKatibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Issa Mahfoudh Haji, amesema Serikali imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika shughuli za uzalishaji za Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa lengo la kuongeza mapato.
  • MH WAZIRI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE KIZIMBANI DOLEWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ameridhishwa na mafanikio ya Maonesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea Dole Kizimbani..
  • WAFANYAKAZI WA OR-TMISEMIMWafanyakazi wa Ofisi Y Rais Tawla Za MIkoa Serikali Za Mitaa Na Idara Maalum Za SMZ Wakiwaaga Watumishi waliomaliza muda wao katika Wizara hiyo.
OR-TAMISEMIM-HABARI

Angali Habari Zote

KATIBU MKUU AKIKATA UTEPE KUZINDUA MAGARI MANNE YA KVZ

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Nd. Issa Mahfoudh Haji amewataka wakufunzi wa Idara maalum za SMZ kuendeleza Mafunzo kwa Vikosi hivyo ili kuwaweka utayari kwa kulinda nchi yao. Ameyasema hayo kwa niab


Read More

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

MHE IDRISSA KITWANA MUSTAFA

Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, akiwahimiza viongozi kushuka chini kwa wananchi na kuacha Ofisi zao ili kusikiliza changamoto. Ameyasema hayo alipokuwa katika muendelezo wa ziara yake katika jimbo la Bumbwini na jimbo la Mahonda Mkoa wa kaskazini Wilaya ya kaskazini B. Aidha, alisisitiza kuwa yeye ni Waziri wa wananchi na ataendelea kutekeleza maelekezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ufanisi ili iwe ni alama ilioachwa na Serikali yao. Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Garlos Nyimbo alisema, wananchi watapata fursa ya kuwasilisha changamoto mbalimbali, zikiwemo zinazohusu wizara hiyo inayohusika pamoja na zile zilizo chini ya Mamlaka za Wizara nyingine, Ili kupatiwa ufumbuzi. Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Juma Sururu Juma, amewahimiza wananchi ushirikiano katika kutambua vipaumbele vya maendeleo ili kutafutiwa suluhisho la changamoto zinazowagusa moja kwa moja. Wananchi wa Jimbo la Bumbwini na jimbo la Mahonda walimpongeza Mhe. Waziri kwa uamuzi wake wa kufika kusikiliza kero zao wakieleza kuwa hatua hiyo inaonesha dhamira ya kweli ya Serikali ya kutatua changamoto zinazowakabili. Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha mawasiliano kati ya Viongozi na Wananchi, pamoja na kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.