KUUNDWA KWA SERIKALI ZA MITAA ZANZIBAR

Serikali za Mitaa zimeanzishwa kwa sharia namba 3 ya mwaka 1986 Zanzibar iliyopitishwa na baraza la wawakili zanzibar, chimbuko la Serikali za mitaa lilianza kwa kuwepo serikali za majimbo zilizozinduliwa rasmin tarehe 4/4/1987 ambapo serikali za majimbo ziligaiwa kwa idadi ya majimbo husika kutoka katika kila Wilaya. Majimbo hayo yalikua yakiongozwa na mwenyekiti wa jimbo anayepatikana kwa njia ya uchaguzi wa kuteuliwa katika chama katika mfumo wa chama kimoja na katibu wa jimbo anateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara.

Majukumu ya serikali za majimboni karibu sawa na majukumu ya serikali za mitaa katika kusaidia miradi ya maendeleo kwa wananchi aidha katika mwaka wa 1995 sheria hiyo ilifutwa na sharia mpya mbili za serikali za mitaa zilianzishwa ambayo ni sharia namba 3 ya mwaka 1995 ilianzisha baraza la manispaa la zanzibar na sharia namba 4 ya mwaka 1995 iliyounda mabaraza ya miji Pemba (Chakechake, Mkoani na Wete) na Halmashauri tisa (9) za Wilaya ambazo ni Magharibi, Kati, Kusini, Kaskazini A na Kaskazini B, kwa upande wa Unguja na Chakechake, Mkoani na Wete kwa upande wa Pemba.

Kuundwa kwa sharia namba 3 ya mwaka 1986 ya serikali za mitaa ilipelekea wilaya ya Konde kubadilishwa jina na kua wilaya ya Micheweni. Aidha mabadiliko hayo yalianzisha wilaya ndogo mbili wilaya ya Tumbatu kwa upande wa Unguja na wilaya ndogo ya Kojani kwa upande wa Pemba. Sharia hii pia ilifanyiwa mapitio tena mwaka 1995 na kupelekea kutenganishwa baina ya majukumu ya baraza la manispaa na halmashauri ya wilaya na mabaraza ya miji sharia namba 3 na 4 za mwaka 1995 za seriakli za mitaa ziliundwa na kupitishwa kwa azma ya kuharakishwa kuwapelekea wananchi mamlaka ya kujiamulia mambo yao wenyewe katika Nyanja za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kifungu cha tatu cha sharia kinaeleza kwamba kila wilaya ya Zanzibar kutakua na halmashauri ambayo itafanyakazi ndani ya eneo la halmashauri, kazi kubwa za halmashauri hizi ni kusaidia seriakli kuu katika mipango yake ya maendeleo kwa wananchi wake, hivyo basi wanadhamana ya kuhakikisha ukusanyaji na utumiaji wa rasilimali na mapato unakwenda vizuri sambamba na kuibua na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

MUUNDO WA SERIKALI ZA MITAA

Baada ya kupitishwa kwa sharia namba 3 na 4 ya mwaka 1995, Idara ya Tawala za Mikoa imepewa jukumu ya kuratibu shughuli zote za maendeleo ya kijamii kupitia taasisi zake za Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya.Taasisi hizo zinaundwa kwa kupatikana kwa waheshimiwa Madiwani ambao wanapatikana kwa njia ya uchaguzi mkuu na watendaji ambao ni waajiriwa wa Serikali kuu.

Kwa upande wa uongozi wa Manispaa, Meya anapatikana kwa kuchaguliwa kupitia madiwani wa eneo la manispaa na mtendaji mkuu wa Baraza la Manispaa ni Mkurugenzi ambaye anateuliwa na Mh. Rais, kwa upande wa Mabaraza ya Miji na Halamshauri za wilaya zinaundwa na waheshimiwa Madiwani kupitia uchaguzi mkuu ambapo Mwenyekiti wa Taasisi hizo anapatikana miongoni mwa madiwani aliechaguliwa na madiwani husika sambamba na mtendaji mkuu wa Taasisi husika ambaye anateuliwa na Mh. Waziri husika mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KWA KUANZISHWA SERIKALI ZA MITAA HADI SASA

Mafanikio mengi yamepatikana tokea kuanzishwa kwa Serikali za Mitaa yakiwemo mafanikio makuu Yafuatayo:

  • Kurekebishwa sheria zilizopo ili zioane na upelekaji wa madaraka ngazi za chini na kutunga sharia kwa ajili ya sekta za serikali za mitaa sharia ambazo pia zitaimarisha utoaji wa huduma.
  • Kuimarisha Huduma za serikali za Mitaa kwa kutoa rasilimali watu zinazohitajika.
  • Kuwepo kwa Majengo mapya ya Serikali za Mitaa yanayokidhi haja katika Serikali za Mitaa.
  • Kuboresha huduma za ukusanyaji taka zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ya Miji.
  • Kuwepo baadhi ya wataalamu katika Taasisi za Serikali za Mitaa.
  • Kuwepo kwa mikakati imara ya Mipango ya Maendeleo ya kila mwaka katika serikali za Mitaa, kama vile kuwasogezea huduma muhimu za kijamii wananchi kama vile kusaidia ujenzi wa vituo vya afya,huduma za elimu,huduma za afya, maji umeme, huduma za barabara ndogo ndogo na baadhi ya maeneo mengineyo ya maendeleo.

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3732119
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
774
219
1835
12964
3732119