TUME YA UTUMISHI YA IDARA MAALUM ZA SMZ.

Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ ni miongoni mwa Tume nne (4) zinazosimamia Utumishi wa Umma, hapa Zanzibar .

Tume hii inasimamia utumishi wa maafisa na askari wa Idara Maalum. Maafisa na askari hawa wanatoka katika Idara Maalum tano (5) nazo ni :-

  1. Kikosi Maalum cha kuzuwia magendo (KMKM)
  2. Jeshi la kujenga Uchumi (JKU)
  3. Chuo cha Mafunzo (MAFUNZO)
  4. Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU)
  5. Kikosi cha Valantia (KVZ).

 

UONGOZI

  • Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Idara Maalum - Col. MIRAJI M. VUAI (mst).
  • Katibu wa Tume ya Utumishi wa Idara Maalum - SSP. HASSAN HAJI HAJI.

 

KAZI ZA TUME YA UTUMISHI

Kama zilivyo Tume nyengine zinazosimamia Utumishi, kazi na uwezo wa Tume umeelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, katika kifungu cha 118, ambacho miongoni mwa kazi hizo ni :-

  1. Kuajiri watu kushika nafasi za utumishi
  2. Kuthibitisha ajira zao za utumishi
  3. Kusitisha au kuachisha utumishi
  4. Kupendekeza Serikalini mishahara na marupurupu ya watumishi
  5. Mamlaka mengine yeyote zitakazopewa kwa mujibu wa sheria iliofungwa na Baraza la Wawakilishi.

Aidha, kifungu cha 36 cha sheria ya utumishi wa umma No 2 ya 2011 kimeeleza kazi na uwezo wa Tume za utumishi, ikiwemo ya Idara Maalum za SMZ.

 

MUUNDO WA TUME

Kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha sheria ya Utumishi wa Umma No 2 ya 2011, Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ inaundwa na Mwenyekiti, ameteuliwa na Raisi wa Zanzibar, muakilishi mmoja wa kila Idara Maalum na wajumbe watatu ambao wanateuliwa na Waziri anayesimamia Idara Maalum za SMZ. Hivyo, Tume imeundwa na Mwenyekiti na wajumbe wanane (8).

Aidha, Tume ina secretariet inayoongozwa na Katibu wa Tume .

 

HISTORIA FUPI YA TUME

Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ iliundwa rasmi mwaka 2011, kabla ya hapo kulikuwepo Tume ya Uajiri ambayo mwenyekiti wake alikuwa Waziri anayesimamia Idara maalum za SMZ na Katibu wa Wizara ndie Katibu wa Tume. Aidha , Wakuu wa Idara Maalum walikuwa wajumbe wa Tume hiyo . utaratibu huu uliendelea hadi mwaka 2011 ilipoundwa sheria ya utumishi wa umma No 2 ya 2011 ambapo Mwenyekiti anateuliwa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Tume ya uajiri ilikuwa insimamiwa na sheria ya Tume ya uajiri No 7  ya 1986 na baadae ilifutwa na sheria ya Tume ya Utumishi ya Idara Maalum No 6 mwaka 2007, ambayo inafanya kazi hadi leo. Hivyo, Tume inafanya kazi kwa kutumia sheria No 6 ya mwaka 2007 na sheria ya Utumishi wa Umma No 2 ya 2011 .

 

VIONGOZI WA TUME

Kama ilivyoelezwa kabla ya mwaka 2011 Mawaziri waliosimamia Idara Maalum walikuwa Wenyeviti wa Tume kwa mfano :- (1-3)

  1. Mhe Iddi Pandu Hassan
  2. Mhe Ali Haji Ali
  3. Mhe Suleiman Nyanga
  4. Miraji M. Vuai (mst)
  5. Said Ali Hamad (mst) (Mwenyekiti wa sasa)

 

SHERIA ZINAZOAMBATANA NA KAZI ZA TUME

  1. Katiba ya Zanzibar ya 1984
  2. Sheria ya Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ No.6 ya 2007 na kanuni zake za 2008
  3. Sheria ya KMKM N0.1 ya 2003
  4. Sheria ya JKU No. 6 ya 2003
  5. Sheria ya Chuo cha Mafunzo No. 1 ya 1980
  6. Sheria Kikosi cha Zimamoto na Uokozi 7 ya 1999
  7. Sheria ya Kikosi cha Valantia No.5 ya 2004
  8. Sheria ya Utumishi wa Umma No.2 ya 2011 na Kanuni zake za 2014

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3713098
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
657
699
6381
16455
3713098