Idara ya uratibu

HUDUMA ZINAZOTOLEWA

  • Idara hii itahusika na majukumu ya uratibu wa serikali za mikoa na serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji wa kazi mbali mbali katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Shehia, kutoa miongozo ya usimamizi katika utekelezaji wa majukumu na kuziwezesha na kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mikoa na Mitaa. Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
  • Majukumu ya Idara
  • i) Kuratibu na kufuatilia shughuli zinazotekelezwa katika ngazi za Mikoa, Wilaya na Shehia;
  • ii) Kuratibu na kufuatilia shughuli zinazotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  • iii) Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutekeleza majukumu yao;
  • iv) Kufuatilia na Kuratibu Mipango ya bajeti ya Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa;
  • v) Kutoa miongozo ya usimamizi na utekelezaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
  • vi) Kuratibu shughuli za kisekta zinazotekelezwa katika Mamlaka za Mikoana Wilaya;
  • vii) Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Mipango ya maendeleo na miradi katika Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa;
  • viii) Kufanya ufuatiliaji na tathmini kwa miradi inayotekelezwa na Serikali za Mitaa katika ngazi ya Wadi na Shehia.

Read More