SERA, SHERIA NA MACHAPISHO.

KUUNDWA KWA SERIKALI ZA MITAA ZANZIBAR

Serikali za Mitaa zimeanzishwa kwa sharia namba 3 ya mwaka 1986 Zanzibar iliyopitishwa na baraza la wawakili zanzibar, chimbuko la Serikali za mitaa lilianza kwa kuwepo serikali za majimbo zilizozinduliwa rasmin tarehe 4/4/1987 ambapo serikali za majimbo ziligaiwa kwa idadi ya majimbo husika kutoka katika kila Wilaya. Majimbo hayo yalikua yakiongozwa na mwenyekiti wa jimbo anayepatikana kwa njia ya uchaguzi wa kuteuliwa katika chama katika mfumo wa chama kimoja na katibu wa jimbo anateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara.

Majukumu ya serikali za majimboni karibu sawa na majukumu ya serikali za mitaa katika kusaidia miradi ya maendeleo kwa wananchi aidha katika mwaka wa 1995 sheria hiyo ilifutwa na sharia mpya mbili za serikali za mitaa zilianzishwa ambayo ni sharia namba 3 ya mwaka 1995 ilianzisha baraza la manispaa la zanzibar na sharia namba 4 ya mwaka 1995 iliyounda mabaraza ya miji Pemba (Chakechake, Mkoani na Wete) na Halmashauri tisa (9) za Wilaya ambazo ni Magharibi, Kati, Kusini, Kaskazini A na Kaskazini B, kwa upande wa Unguja na Chakechake, Mkoani na Wete kwa upande wa Pemba.

Kuundwa kwa sharia namba 3 ya mwaka 1986 ya serikali za mitaa ilipelekea wilaya ya Konde kubadilishwa jina na kua wilaya ya Micheweni. Aidha mabadiliko hayo yalianzisha wilaya ndogo mbili wilaya ya Tumbatu kwa upande wa Unguja na wilaya ndogo ya Kojani kwa upande wa Pemba. Sharia hii pia ilifanyiwa mapitio tena mwaka 1995 na kupelekea kutenganishwa baina ya majukumu ya baraza la manispaa na halmashauri ya wilaya na mabaraza ya miji sharia namba 3 na 4 za mwaka 1995 za seriakli za mitaa ziliundwa na kupitishwa kwa azma ya kuharakishwa kuwapelekea wananchi mamlaka ya kujiamulia mambo yao wenyewe katika Nyanja za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kifungu cha tatu cha sharia kinaeleza kwamba kila wilaya ya Zanzibar kutakua na halmashauri ambayo itafanyakazi ndani ya eneo la halmashauri, kazi kubwa za halmashauri hizi ni kusaidia seriakli kuu katika mipango yake ya maendeleo kwa wananchi wake, hivyo basi wanadhamana ya kuhakikisha ukusanyaji na utumiaji wa rasilimali na mapato unakwenda vizuri sambamba na kuibua na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

MUUNDO WA SERIKALI ZA MITAA

Baada ya kupitishwa kwa sharia namba 3 na 4 ya mwaka 1995, Idara ya Tawala za Mikoa imepewa jukumu ya kuratibu shughuli zote za maendeleo ya kijamii kupitia taasisi zake za Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya.Taasisi hizo zinaundwa kwa kupatikana kwa waheshimiwa Madiwani ambao wanapatikana kwa njia ya uchaguzi mkuu na watendaji ambao ni waajiriwa wa Serikali kuu.

Kwa upande wa uongozi wa Manispaa, Meya anapatikana kwa kuchaguliwa kupitia madiwani wa eneo la manispaa na mtendaji mkuu wa Baraza la Manispaa ni Mkurugenzi ambaye anateuliwa na Mh. Rais, kwa upande wa Mabaraza ya Miji na Halamshauri za wilaya zinaundwa na waheshimiwa Madiwani kupitia uchaguzi mkuu ambapo Mwenyekiti wa Taasisi hizo anapatikana miongoni mwa madiwani aliechaguliwa na madiwani husika sambamba na mtendaji mkuu wa Taasisi husika ambaye anateuliwa na Mh. Waziri husika mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KWA KUANZISHWA SERIKALI ZA MITAA HADI SASA

Mafanikio mengi yamepatikana tokea kuanzishwa kwa Serikali za Mitaa yakiwemo mafanikio makuu Yafuatayo:

  • Kurekebishwa sheria zilizopo ili zioane na upelekaji wa madaraka ngazi za chini na kutunga sharia kwa ajili ya sekta za serikali za mitaa sharia ambazo pia zitaimarisha utoaji wa huduma.
  • Kuimarisha Huduma za serikali za Mitaa kwa kutoa rasilimali watu zinazohitajika.
  • Kuwepo kwa Majengo mapya ya Serikali za Mitaa yanayokidhi haja katika Serikali za Mitaa.
  • Kuboresha huduma za ukusanyaji taka zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ya Miji.
  • Kuwepo baadhi ya wataalamu katika Taasisi za Serikali za Mitaa.
  • Kuwepo kwa mikakati imara ya Mipango ya Maendeleo ya kila mwaka katika serikali za Mitaa, kama vile kuwasogezea huduma muhimu za kijamii wananchi kama vile kusaidia ujenzi wa vituo vya afya,huduma za elimu,huduma za afya, maji umeme, huduma za barabara ndogo ndogo na baadhi ya maeneo mengineyo ya maendeleo.

Afisi kuu Unguja


Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ

P.O BOX 4220

Vuga - Zanzibar

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

Afisi ya Pemba


Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ Pemba

P.O BOX 04

Chakechake - Pemba

Tel: +255242452768

Fax: +255242452768

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

MUUNDO WA MIKOA

Mara tu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, miundo ya Mikoa ilibadilika kwa azma ya kusogeza huduma kwa wananchi. Kiutawala Zanzibar iligaiwa katika mikoa mitatu (3) ambapo Kisiwa cha Unguja kilikua na Mikoa 2 ambayo ni Mkoa wa Mjini ukiongozwa na Mheshimiwa Saidi Washoto na Mkoa wa Shamba ambao ulikua ukiongozwa na Mheshimiwa Suleiman Ameir (Mrembo). Pemba ilikua chini ya Mkoa mmoja ambao uliitwa mkoa wa Pemba ukiongozwa na Mheshimiwa Rashid Abdallah, Aidha kwa upande wa upande wa Unguja kulianzishwa Wilaya sita (6) nazo ni Makunduchi baadae ikawa Wilaya ya Kusini, Chwaka baadae ikawa Wilaya ya Kati. Bumbwini baadae ikawa Wilaya ya Kaskazini B, Mkokotoni baadae ikawa Wilaya ya Kaskazini A. Wilaya ya Mjini ilibaki kama ilivyo na wilaya ya Mfenesini baadae ikawa wilaya ya Magharibi. Majina yote ya Wilaya ndio yalikua makao makuu ya Wilaya hizo ambazo kabla ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 ndio yalikua Makao ya Mudiri.

Kwa upande wa kisiwa cha Pemba kulikua na Wilaya nne ambazo ni: Wilaya ya Wete, Wilaya ya Konde, Wilaya ya Chakechake na Wilaya ya Mkoani. Baadae mapema katika miaka ya 70 Wilaya ya Konde ikahamishiwa Wilaya ya Micheweni kwa lengo la kuharakisha ustawi wa maendeleo ya jamii husika.

Mwanzoni mwa miaka ya 70 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianzisha Mikoa ilianzisha Mikoa Mitano (5) ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mkoa wa Kusini Pemba. Kila mkoa ulikua umegawika katika wilaya mbili ili Selikali za Mikoa ziweze kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera miongozo na Maagizo ya Serikali kwa karibu zaidi.

Sambamba na mabadiliko hayo, katika mwaka 1998 Serikali ilipitisha sharia Namba 1 ya mwaka 1998 ya Mamlaka ya Serikali za mikoa ambayo ilifafanua zaidi juu ya kazi na majukumu ya wakuu wa Wilaya, pamoja na maofisa Tawala wa Mikoa na Wilaya. Sheria hiyo iliunda kamati za maendeleo za mikoa (Regianal Development Commitees) ambazo zimepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendelea katika ngazi husika.

Aidha sharia hiyo, imerejesha utawala wa Masheha ambao wanateuliwa na Mkuu wa Mkoa baada ya kushauriana na Mkuu wa Wilaya husika. Kwa mujibu wa sharia hiyo sheha ndio mtendaji mkuu wa Serikali katika ngazi ya chini ya Utawala. Aidha, katika utendaji wake, Sheha huwa anasaidiwa na Baraza la Ushauri wa shehia ambalo linaundwa na wajumbe wasiozidi 12.

Idadi ya shehia zilizopo sasa ni 335 (214 kwa Unguja na 121 kwa Pemba) zilizoanzishwa chini ya sharia hii.

MAJUKUMU YA MAMLAKA YA MIKOA.

Majukumu makuu ya mamlaka za mikoa ni kama yafuatayo;

  • Kwa mujibu wa sharia namba 5/1998 ya Tawala za mikoa Zanzibar, Mamlaka za Serikali za mikao zimepewa jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Seriakli katika maeneo ya utawala. Aidha, mamlaka hizo zimepewa jukumu la kutoa miongozo, kutafsiri sera sharia na kuhakikisha uendelevu wa hali ya amani na utulivu katika Mikoa.
  • Mikoa ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya na Shehia zilizomo katika Mikoa. Aidha Mikoa ina jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama pamoja na kutatua masuala/matatizo mbalimbali ya wananchi katika Mikoa husika.
  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa malengo ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, maji, miundo mbinu, utawala Bora, umeme ustawi wa jamii maendeleo ya vijana ,wanawake na watoto, uvuvi, ufugaji maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  • Kuratibu shughuli mtambuka zikiwemo UKIMWI, jinsia madawa ya kulevya, utawala bora, maswala ya watu wenye ulemavu na mazingira.

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3724073
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
9
580
2328
4918
3724073