OFISI YA MRAJISI WA JUMUIYA ZISIZO ZA SERIKALI ZANZIBAR

Nini maana ya Jumuiya Zisizo za Kiserikali.

Jumuiya za kiraia ni taasisi binafsi za hiyari zinazoanzishwa kwa lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo hasa katika maeneo ambayo hayajafanyiwa kazi. Sheria ya Jumuiya No. 6 ya mwaka 1995 ndio inayotumika kuongoza usajili pamoja na kuweka masharti na utaratibu wa usimamizi na uendeshaji wa Jumuiya za hiari.

Aina za Jumuiya za kiraia Jumuiya za kiraia zinaweza kuwekwa katika makundi mbalimbali kutokana na muundo wa Jumuiya, maeneo ya kazi, shughuli inazozifanya au eneo (nchi) la awali ilipoundwa. Jumuiya za kiraia zinaweza kuwa:

  1. Kamati za maendeleo (Community Based Organization – CBOs) hizi ni Jumiya zinazoanzishwa kwa lengo la kufanya kazi katika eneo maalum (lisilozidi wilaya moja)
  2. Za kitaifa (local NGOs) hizi ni taasisi zinazofanya kazi zake ndani ya nchi moja tu.
  3. Za kimataifa (International NGOs) hizi ni zile zinazofanya kazi zake kimataifa (ndani ya nchi zaidi ya moja).

Sifa za Jumuiya zinazosajiliwa Kwa mujibu wa sheria taasisi yoyote inayotaka kusajiliwa kama Jumuiya ya kiraiya Zanzibar ni lazima

  1. Iweni taasisi ya hiyari: kuanzishwa kwake kutokana na hiyari ya waanzilishi wenyewe na kusiwe kwa kulazimishwa ama kutezwa nguvu.
  2. Isijuhusishe na mabo ya kisiasa: kuanzishwa kwa taasisi hakutakiwi kuwe na lengo la kisiasa kama vile kushiriki au kushabikia katika kampeni ya chama Fulani au mgombea Fulani.
  3. Ianzishwe kwa kunufaisha jamii: lengo la kuanzishwa kwake liwe ni kwa maslahi ya jamii inayohusika isiwe kwa maslahi au kutatua matatizo ya mtu binafsi au famulia fulani.

Muda wa kusajili Jumuiya za Kiraia Kwa mujibu wa kifungu nambari 10 cha Sheria ya Jumuiya kila taasisi iliyoanzishwa Zanzibar italazimika kuwasilisha maombi ya usajili kwa Mrajis wa Jumuiya za Kiraia ndani ya siku 28 kuanzia siku ilipoanzishwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

Umuhimu wa kusajili Jumuiya za Kiraia Jumuiya za kiraia iliyosajiliwa ina uwezo wa

  1. Kutambulika uwepo wake kisheria
  2. Kupata ruzuku na misaada mengine kiurahisi
  3. Kupata misamaha katika kodi mbalimbali
  4. Kuendesha shughuli zake bila woga
  5. Kuwa na uhusiano mzuri na Serikali pamoja na taasisi nyengine

Matatizo yanayoweza kutokea kwa Jumuiya zisizosajiliwa Jumuiya zisizosajiliwa hukosa

  1. Kutambulika kisheria suala ambalo linaweza kusababisha kukosekana fursa mbalimbali kama vile kuingia katika mikataba.
  2. Uhalali wa uwepo wake husika kisheria.
  3. Fursa ya kufungua akaunti ya Jumuiya.
  4. Fursa ya kutambuliwa kwa taasisi kitaifa na kimataifa na kupelekea kukosa misaada.
  5. Misamaha mbalimbali kwa Serikali mfano msamaha wa kodi n.k

Wajibu wa taasisi iliyosajiliwa

  1. Kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa katiba na kanuni.
  2. Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji na fedha za kila mwaka kwa Mrajis wa Jumuiya za kiraia.
  3. Kuwa na anuani na afisi inayotambulika.
  4. Kuwasilisha mabadiliko yaliofanywa na taasisi kwa Mrajis.
  5. Kuwa na buku la usajili wa wanachama na mahesabu ya taasisi.
  6. Taasisi inatakiwa iweke utaratibu wa ukaguzi wa mahesabu.

NB. Taasisi yoyote itakayovunjika haitotakiwa kuzigawa mali zinazomilikiwa na taasisi hiyo kwa wanachama wake badala yake i tatakiwa kwa kushirikiana na Mrajis wa Jumuiya za kiraia na mara baada ya kulipa madeni inayodaiwa taasisi hiyo kuzipeleka mali hizo kwa taasisi nyengine, lengo ni kuweza kuendelea kutumika kwa huduma za kijamii.

Fika Ofisi ya Mrajis kusajili Jumuiya na Vielelezo vifuatavyo :-

Kila Jumuiya inapaswa kuwakilisha mambo yafuatayo kwa ajili ya usajili:

  1. Katiba na kanuni za Jumuiya husika
  2. Fomu ya maombi ya usajili itakayokuwa na taarifa za Jumuiya kwa ukamilifu
  3. Orodha ya majina ya wanachama Jumuiya za kigeni zinazotaka kufunguwa tawi Zanzibar

Pamoja na kufuata taratibu zilizotajwa hapo juu pia zitawasilishwa.

  1. Taarifa binafsi (CV) za viongozi wa Jumuiya
  2. Vivuli vya passipoti (kwa wasiokuwa Watanzania)
  3. Kivuli cha kitambulisho kwa Wazanzibari
  4. Kumbukumbu ya kikao kilichoamua kufungua tawi Zanzibar
  5. Barua ya kuteua mwakilishi wa Jumuiya katika usajili wa tawi Zanzibar
  6. Barua ya utambulisho kutoka kutoka Tanzania Bara kwa Jumuiya zinazotaka kuja kufanya kazi Zanzibar.

kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia anuani zifuatazo:

Ofisi ya RaisTawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

P.O BOX 4220 Vuga - Zanzibar

Tel: +255242230034 Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. www.tamisemim.go.tz

OFISI YA AFISA MDHAMINI - ORTMSMIM (OFISI KUU PEMBA)

Ofisi ya Afisa Mdhamini ni kiungo kati ya Taasisi za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ zilizopo Pemba ikiwa na jukumu kuu la kuratibu na kusimamia kazi zote za Ofisi kwa upande wa Pemba.

 

 UONGOZI

Kiongozi mkuu (Afisa Mdhamini) wa shughuli za ORTMSMIM kwa upande wa Pemba niNd. THABIT OTHMAN ABDALLA 

MAJUKUMU YA OFISI YA AFISA MDHAMINI (KWA UPANDE WA PEMBA)

  • Kuratibu shughuli zote zinazofanywa na ORTMSMIM.
  • Kuratibu na kuwasilisha ripoti au taarifa za utekelezaji za kila robo, nusu na mwaka kwa Katibu Mkuu wa ORTMSMIM.
  • Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
  • Kuratibu taarifa za bajeti na hotuba ya makadario ya mapato na matumizi.
  • Kuratibu,kushauri,kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Serikali za mitaa na Mamlaka zake.
  • Kufuatilia na kukagua utendaji wa Serikali za Mitaa katika kutoa huduma.
  • Kuimarisha utawala bora na kuimarisha uwezo wa Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma.

IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

UONGOZI

Mkurugenzi katika idara ya mipango sera na utafiti ni ndugu ABDALLAH ISSA MGONGO.

KAZI KUU

  • Kuratibu na kusimamia mipango inayoendeshwa na Wizara.
  • Kuunda na kuratibu sera na sheria.
  • Kupanga, kubuni na kusimamia miradi na programu.
    Kuandaa mipango ya kila mwaka, kuweka mikakati na bajeti ya kila mwaka ya Wizara.
  • Kuratibu shughuli za utafiti wa Wizara na kuandaa ripoti ya utafiti.
  • Kukagua, kuimarisha na kuratibu mipango na programu za maendeleo ya wizara.
  • Kupitia na kutathmini utekelezaji wa sera, mipango, mipango na mradi ya wizara.

Kuratibu, kufuatilia na kusimamia miradi na programu inayofadhiliwa

IDARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.

MAJUKUMU YA IDARA

  1. Kuratibu shughuli zote za mikoa na serikali za mitaa.
  2. kusimamia sera na sheria katika Mikoa na Serikali za mitaa
  3. Kusimamia utekelezaji wa Mamlaka zaMikoa na Serikali za mitaa
  4. kufanya ufatiliaji wa Majukumu ya mamlaka za Serikali za Mitaa.

IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI:

MUUNDO
ORG3

1. MKURUGENZI
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi ni Ndugu JUMA NYASA JUMA.

MAJUKUMU

  • Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali Watu na Utawala kwa wizara husika. 
  • Kusimamia makujumu ya vitengo vilivyo chini ya Idara.
  • Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Wizara.
  • Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji.
  • Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum.
  • Kuratibu masuala mtambuka yakiwemo (Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya  hali ya nchi, mambo ya idadi ya watu).
  • Kutoa huduma za kitaalamu na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwa ajili ya Idara nyengine.
  • Kutoa huduma za uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na matumizi, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni.
  • Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara.
  • Kuandaa na kusimamia bajeti ya Idara.
  • Kufanya kazi nyenginezo kama zitakavyoelekezwa na Uongozi wa Wizara kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za kazi.

2. KITENGO CHA UENDESHAJI
Kinaongozwa na Ofisa Utawala Mkuu.

MAJUKUMU

  • Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi. 
  • Kusaidia kusimamia nidhamu  ya wafanyakazi.
  • Kuainisha matatizo ya wafanyakazi.
  • Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya wizara ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano.
  • Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.
  • Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara.
  • Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi. 

3. KITENGO CHA UTUMISHI
Kinaongozwa na Ofisa Mkuu Utumishi.

MAJUKUMU

  • Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote kulingana na mahali alipo. 
  • Kukusanya takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
  • Kusaidia kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
  • Kufanya kazi zote atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

4. KITENGO CHA UTUNZAJI KUMBUKUMBU
Kinaongozwa na Ofisa Kumbukumbu Mkuu.

MAJUKUMU

  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji. 
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk.) katika mafaili.
  • Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
  • Kufanya kazi nyengine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi. 

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

3724244
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
180
580
2499
5089
3724244