WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII ZANZIBAR.

Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (The Zanzibar Civil Status Registration Agency) imeanzishwa kwa sheria namba 3 ya mwaka 2018 iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kutiwa saini na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tarehe 2/01/2018 na kuwa Sheria rasmi. Sheria hiyo imetangazwa na Mheshimiwa Waziri wa nchi OR Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika Gazeti rasmi la Serikali na kuanza kutumika tarehe 5/2/2018.

MAJUKUMU YA OFISI (ZCSRA):

  1. Kupokea taarifa kutoka Taasisi zinazohusika (Shehia, Hospitali, Uhamiaji, Mahkama ya Kadhi, Taasisi za dini, Imani na Madhehebu mbali mbali)
  2. Kuthibitisha taarifa ambazo zinahusiana na Matukio ya Kijamii na Kuzisajili.
  3. Kuhifadhi Rejista zote katika mfumo wa kielektroniki.
  4. Kutengeneza, kusimamia, kutunza na kuendeleza  Rejista  za  Matukio  ya  Kijamii.
  5. Kutoa Shahada maalum (cheti) na Kitambulisho kulingana na maombi ya mhusika  na  kwa  mujibu  wa  Sheria  husika.
  6. Kutoa Namba ya Upekee ambayo haitoweza kutumika tena kwa mtu yeyote maishani.
  7. Kuziunganisha taarifa kutoka katika mifumo (Data Base) mingine ya kiserikali inayohusiana na Matukio ya Kijamii.

MATUKIO YA KIJAMII:

    1. Matukio ya Kijamii maana yake, ni kumbukumbu za Matukio ambayo yanahifadhiwa katika Mamlaka za serikali zikijumuisha Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Utambulisho.
    2. Matukio yote haya yanasajiliwa na kutolewa shahada au vitambulisho maalum ikiwa ni uthibitisho.
    3. Mfumo wa Usajili unaotumika ni wa Kielektroniki badala ya wa njia ya kawaida.
    4. Shahada ya Utambulisho itatolewa kwa Wazanzibari na wasiokuwa Wazanzibari kwa mujibu wa masharti ya kifungu Na. 27 cha sheria Na. 3 ya 2018.

Kwa maelezo Zaidi wasiliana na:-

WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII ZANZIBAR

ZANZIBAR CIVIL STATUS REGISTRATION AGENCY (ZCSRA)

P.O.Box: 264, Migombani, Zanzibar. Tel: +255 777978733

Website/Tovuti: www.zcsra.go.tz     Email/Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.