Afisi kuu Unguja
Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ
P.O BOX 4220
Vuga - Zanzibar
Tel: +255242230034
Fax: +255242230034
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Afisi ya Pemba
Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ Pemba
P.O BOX 04
Chakechake - Pemba
Tel: +255242452768
Fax: +255242452768
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
TUME YA UTUMISHI YA IDARA MAALUM ZA SMZ.
Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ ni miongoni mwa Tume nne (4) zinazosimamia Utumishi wa Umma, hapa Zanzibar .
Tume hii inasimamia utumishi wa maafisa na askari wa Idara Maalum. Maafisa na askari hawa wanatoka katika Idara Maalum tano (5) nazo ni :-
- Kikosi Maalum cha kuzuwia magendo (KMKM)
- Jeshi la kujenga Uchumi (JKU)
- Chuo cha Mafunzo (MAFUNZO)
- Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU)
- Kikosi cha Valantia (KVZ).
UONGOZI
- Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Idara Maalum - Col. MIRAJI M. VUAI (mst).
- Katibu wa Tume ya Utumishi wa Idara Maalum - SSP. HASSAN HAJI HAJI.
KAZI ZA TUME YA UTUMISHI
Kama zilivyo Tume nyengine zinazosimamia Utumishi, kazi na uwezo wa Tume umeelezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, katika kifungu cha 118, ambacho miongoni mwa kazi hizo ni :-
- Kuajiri watu kushika nafasi za utumishi
- Kuthibitisha ajira zao za utumishi
- Kusitisha au kuachisha utumishi
- Kupendekeza Serikalini mishahara na marupurupu ya watumishi
- Mamlaka mengine yeyote zitakazopewa kwa mujibu wa sheria iliofungwa na Baraza la Wawakilishi.
Aidha, kifungu cha 36 cha sheria ya utumishi wa umma No 2 ya 2011 kimeeleza kazi na uwezo wa Tume za utumishi, ikiwemo ya Idara Maalum za SMZ.
MUUNDO WA TUME
Kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha sheria ya Utumishi wa Umma No 2 ya 2011, Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ inaundwa na Mwenyekiti, ameteuliwa na Raisi wa Zanzibar, muakilishi mmoja wa kila Idara Maalum na wajumbe watatu ambao wanateuliwa na Waziri anayesimamia Idara Maalum za SMZ. Hivyo, Tume imeundwa na Mwenyekiti na wajumbe wanane (8).
Aidha, Tume ina secretariet inayoongozwa na Katibu wa Tume .
HISTORIA FUPI YA TUME
Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ iliundwa rasmi mwaka 2011, kabla ya hapo kulikuwepo Tume ya Uajiri ambayo mwenyekiti wake alikuwa Waziri anayesimamia Idara maalum za SMZ na Katibu wa Wizara ndie Katibu wa Tume. Aidha , Wakuu wa Idara Maalum walikuwa wajumbe wa Tume hiyo . utaratibu huu uliendelea hadi mwaka 2011 ilipoundwa sheria ya utumishi wa umma No 2 ya 2011 ambapo Mwenyekiti anateuliwa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Tume ya uajiri ilikuwa insimamiwa na sheria ya Tume ya uajiri No 7 ya 1986 na baadae ilifutwa na sheria ya Tume ya Utumishi ya Idara Maalum No 6 mwaka 2007, ambayo inafanya kazi hadi leo. Hivyo, Tume inafanya kazi kwa kutumia sheria No 6 ya mwaka 2007 na sheria ya Utumishi wa Umma No 2 ya 2011 .
VIONGOZI WA TUME
Kama ilivyoelezwa kabla ya mwaka 2011 Mawaziri waliosimamia Idara Maalum walikuwa Wenyeviti wa Tume kwa mfano :- (1-3)
- Mhe Iddi Pandu Hassan
- Mhe Ali Haji Ali
- Mhe Suleiman Nyanga
- Miraji M. Vuai (mst)
- Said Ali Hamad (mst) (Mwenyekiti wa sasa)
SHERIA ZINAZOAMBATANA NA KAZI ZA TUME
- Katiba ya Zanzibar ya 1984
- Sheria ya Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ No.6 ya 2007 na kanuni zake za 2008
- Sheria ya KMKM N0.1 ya 2003
- Sheria ya JKU No. 6 ya 2003
- Sheria ya Chuo cha Mafunzo No. 1 ya 1980
- Sheria Kikosi cha Zimamoto na Uokozi 7 ya 1999
- Sheria ya Kikosi cha Valantia No.5 ya 2004
- Sheria ya Utumishi wa Umma No.2 ya 2011 na Kanuni zake za 2014
Osifi ya Raisi Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ inatangaza Zabuni ya usambazaji wa vifaa vya ofisi.
Kufuatia kufanyiwa marekebisho kwa Wizara za Serikali, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ iliundwa mnamo mwezi wa Agosti 2013 baada ya kuunganishwa kwa baadhi ya Idara kutoka taasisi nyengine za Wizara.
Kufuatia kufanyiwa marekebisho kwa Wizara za Serikali, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ iliundwa mnamo mwezi wa Agosti 2013 baada ya kuunganishwa kwa baadhi ya Idara kutoka taasisi nyengine za Wizara.
IDARA YA URATIBU IDARA MAALUM
Ofisi ya Uratibu Idara Maalum za SMZ inajukumu la kuratibu na kusimamia kazi za Idara Maalum za SMZ zikiwemo za utekelezaji wa sera mipango mikakati ya maendeleo, tafiti pamoja na kutoa miongozo kwa Idara Maalum na usimamizi wa Mahakama ya Rufaa za Idara Maalum za SMZ.
Aidha Idara inajukumu la kisera kwa kushirikiana na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ juu ya masuala ya kiutumishi maslahi kuwajengea uwezo maafisa na wapiganaji kiutendaji na kuratibu masuala ya mashirikiano ya kiulinzi, kimichezo, operation maalum na mafunzo ya pamoja na utekelezaji wa maelekezo yote yatakayotolewa na Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ.
HISTORIA FUPI YA OFISI YA URATIBU
Ofisi ya Uratibu Idara Maalum za SMZ ilianzishwa mnamo miaka ya 1980 ambayo shughuli zake zikisimamiwa na mratibu Idara Maalum tokea kuanzishwa kwake hadi mwaka 2017, Ofisi hii imekuwa ikiongozwa na mratibu ambae huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Idara Maalum za SMZ kwa mujibu wa sheria.
Kuanzia tarehe 2/10/2017 kwa mara ya kwanza uteuzi wa kiongozi wa Ofisi hii ulifanywa kwa mamlaka ya Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi chini ya kifungu cha 53 (a) cha katiba ya Zanzibar na kifungu cha 12 (2) cha sheria ya Utumishi wa Umma.
UONGOZI
Mratibu wa Idara ya Uratibu wa Idara Maalum ni: ...................
MAJUKUMU YA IDARA YA URATIBU
Mabadiliko haya ya mamlaka ya uteuzi wa kiongozi wa ofisi hii yanalazimisha kutathiminiwa upya kwa kazi za ofisi zinazofanywa hivi sasa ili ziendane na hali ya ofisi kulingana na taasisi sahihi ya majukumu ya Idara Maalum za SMZ.
Ofisi ya Uratibu ya Idara Maalum za SMZ kwa sasa inamajukumu yafuatayo:
- Kuratibu mafunzo ya kiulinzi na kiusalama ndani na nje ya nchi.
- Kuratibu mahusiano na mashirikiano kwa vyombo vya kiulinzi na kiusala baina ya SMT na SMZ.
- Kufanya uperesheni maalum kwa kazi za ulinzi na ujenzi wa taifa.
- kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo mikakati,sera,miongozo ya bajeti na tafiti za Idara Maalum pamoja na kutoa miongozo ya Serikali kwa Idara Maalum kwa idhini ya Wizara.
- Kuratibu uandaaji na ushiriki wa michezo kwa upande wa kanda ya Zanzibar BAMATA.
- Kuratibu program za mafunzo ya muda na mrefu kwa viongozi maafisa na maaskari kwa kushirikiana na Idara husika.
- Kupokea na kusimamia maelekezo na maagizo yeyote yanayohusu Idara Maalum kutoka kwa Kamanda Mkuu wa Idara Maalum.