Mnamo Tarehe 19, Novemba 2020 Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alitangaza Muundo wa Wizara pamoja na Baraza la Mawaziri, ambapo alimteuwa Mheshimiwa Massoud Ali Mohammed (Mwakilishi wa wananchi Jimbo la Ole) kuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ (OR-TMSMIM).
Muundo wa Afisi hii unajumuisha Afisi za Wakuu wa Mikoa, Afisi za Wakuu wa Wilaya, Jiji, Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri.
Kadhalika Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii, Afisi ya Asasi na Jumuiya zisizokuwa za Serikali (NGO's), Viwanda vya Idara Maalum za SMZ, pamoja na Idara Maalum za SMZ ambazo ni:-
1. Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM).
2. Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKUZ).
3. Idara ya Chuo cha Mafunzo (MF).
4. Idara ya Zimamoto na Uokozi (KZU).
5. Idara ya Valantia (KVZ).
Aidha kwa mujibu wa ibara ya 123(1) Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Ambapo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ndie msimamizi wa Afisi inayosimamia Idara Maalum za SMZ.
Katika kutekeleza malengo ya uanzishwaji wa Wizara hii Afisi itahakikisha misingi ya uwajibikaji, uwazi, ufanisi na kujitolea katika ngazi zote za uongozi wa Wizara.
HISTORIA
Kabla ya Mapinduzi ya januari 1964, wananchi walikua hawashirikishwi katika katika maamuzi kuhusu ustawi wa maendeleo yao. Mtiririko wa ngazi za utawala ulikua ni wa kupokea amri na kusimamia utelezaji wa amri hizo ambazo huanzia ngazi ya juu ya...
Dira
Kuwa taasisi imara katika kusimamia amani, usalama, usajili wa wakaazi na upatikanaji wa huduma karibu na wananchi.
Dhamira
Kujenga mazingira mazuri ya ushiriki wa wananchi katika kudumisha amani ulinzi wa mali zao, kuimarisha huduma za kijamii, kuhakikisha kuwa jamii inashiriki katika kupanga na kusimamia shughuli za maendeleo katika maeneo yao kwa kuzingatia misingi ya utawala bora ikihusisha kuwatambua wakaazi wa maeneo husika na utambulisho wao.
Majukumu
Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ ina majukumu makuu yafuatayo:-
- Kusimamia Sera, Sheria na Kanuni mbali mbali za Ofisi.
- Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo