Super User

Super User

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, imefanya maamuzi ya kurudisha majukumu ya utekelezaji katika wizara husika kwa sekta zilizokuwa kwenye mfumo wa Ugatuzi.

Uamuzi huo wa serikali umezingatia zaidi changamoto ambazo zilijitokeza wakati wa utoaji huduma, pamoja Na kupata maoni ya wadau hasa wapokea huduma Na watumishi wa umma wanaotekeleza mfumo wa Ugatuzi.

Akizungumza Na vyombo vya habari Afisini kwake Vuga, Waziri wa nchi Afisi ya Rais Tawala za mikoa serikali za mitaa Na Idara maalum za SMZ MH Masoud Ali Mohamed, amesema makabidhiano ya sekta hizo ambazo ni kilimo, Afya Na Elimu kurudi katika Wizara zao yanatarajiwa kufanyika mwezi julai 2021.

Aidha MH Masoud amewahakikishia wananchi kuwa utoaji wa huduma utaendelea kama kawaida na kuzitaka serikali za mitaa ambazo ni mabaraza ya Miji, Manispaa Na Halmashauri za wilaya kusimamia mambo ya msingi ikiwemo usafi wa Miji Na kutoa tozo stahiki kwa wafanyabiashara kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Pia MH Masoud ameutaka uongozi wa Idara maalum za SMZ kushirikiana na Manispaa katika suala la usafi na kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

FAMILIA YA ALIYEKUWA RAIS WA AWAMU YA PILI ZANZIBAR MAREHEMU ABOUD JUMBE MWINYI, IMEUNGANA NA VIONGOZI WA SERIKALI KATIKA DUA MAALUM YA KUMUOMBEA KIONGOZI HUYO.
AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO ILIYOFANYIKA KWENYE MAKAAZI YA FAMILIA HIYO MIGOMBANI, WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ, MHE. MASOUD ALI MOHAMED, AMESEMA UTARATIBU HUO UNAWAKUMBUSHA WANANCHI KUTAMBUA NA KUTHAMINI JITIHADA ZILIZOFANYWA NA VIONGOZI WALIOPITA.
AMESEMA VIONGOZI HAO WAMETUMIA MUDA WAO KATIKA KUIMARISHA MAENDELEO YA TAIFA NA KUJALI MASLAHI YA WANANCHI WAKE, HIVYO KUNA KILA SABABU YA KUWAKUMBUKA NA KWAOMBEA DUA IKIWA NI SEHEMU YA KUWAENZI NA KUYAENDELEZA MEMA WALIYOYAANZISHA.
AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA FAMILIA, ND. RAJAB ABOUD JUMBE, AMEPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUWAENZI VIONGOZI WALIOPITA KWANI INAIMARISHA UKARIBU KATI FAMILIA NA SERIKALI.
DUA HIYO IMEFANYIKA IKIWA NI KUELEKEA SIKU YA KUMBUKUMBU YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MAREHEMU ABEID AMANI KARUME IFIKAPO APRILI 7 YA KILA MWAKA.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 jumbe1  jumbe2
 DUA  FAMILIA YA ALIYEKUWA RAIS WA AWAMU YA PILI ZANZIBAR MAREHEMU ABOUD JUMBE MWINYI
 jumbe3  jumbe4
 DUA  DUA
 jumbe5  
 DUA  

Wakulima 135 waliouza zao la miwa msimu huu wakabidhiwa kiasi cha 300,000,000/= kutoka Kiwanda cha Sukari Mahonda Zanzibar, ambapo Chuo cha Mafunzo Zanzibar kimepata hundi ya milioni hamsini (50,000,000/=).

Akikabidhi hundi kwa wakulima binafsi pamoja na Jehi la Kujenga Uchumi JKUZ na Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMIM Mhe. Masoud Ali Mohammed amewaomba wananchi kuona umuhimu wa kubadilika na kuzalisha zao la miwa kwani lina tija na soko la uhakika

Aidha amesema uwekezaji wa kiwanda hicho hupeleka kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kuimarisha soko la ndani, hivyo ameagiza kwa Idara Maalum za SMZ kujitathmini na kuangalia uwezekano wa kuyatumia maeneo ya kilimo kwa kuimarisha wakulima wa miwa.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 1 kiwanda miwa  2 kiwanda miwa
   

Kukamilika haraka kwa matengenezo ya jengo la biashara la Michenzani Mall kutawawezesha wafanyabiashara kuutumia vyema msimu wa sikukuu.

Akikagua kazi za matengenezo zinazoendea Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Nd. Mahmoud Mohd Mussa, amesema wananchi na wafanyabiashara wamekuwa na matumaini ya kulitumia jengo hilo la kisasa ambalo limekusudiwa kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya biashara hapa nchini.

Bi Safia khalfan ambae ni meneja majengo wa kampuni ya knight Frank inayofanya matengenezo amesema kiwango cha bei ya kukodisha milango kimezingatia uhalisia wa jengo hilo na tayari wafanyabiasha wameshajitokeza kuomba nafasi za kuendesha shughuli zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Zanzibar Said Salmin Ufuzo amesema kufanyika kwa biashara katika eneo hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi walio wengi. .... BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 meya1 meya2 
 Michenzani Mall (Muonekano wa nje)  Michenzani Mall (Muonekano wa ndani)
 meya3  meya4
 Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Nd. Mahmoud Mohd Mussa  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Zanzibar Said Salmin Ufuzo
 meya5  meya6
 Bi Safia khalfan Meneja majengo wa kampuni ya Knight Frank  Michenzani Mall
 meya7  meya8
 Michenzani Mall  Michenzani Mall

Mahkama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ imetakiwa kusimamia katika kutoa maamuzi bila ya hofu ili kuwatendea haki wapiganaji wanaopeleka malalamiko yao.

Akizungumza na wajumbe wa Mahkama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za mikoa serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed ameitaka Mahkama hiyo kushughulikia rufaa zinazowasilishwa na kuzipatia ufumbuzi.

Aidha ameiomba Mahkama hiyo kuwa na ushirikiano na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ  ili kurahisisha masuala ya kiutendaji na kupunguza idadi ya kesi.

Mwenyekiti wa Mahkama ya rufaa ya Idara maalum za SMZ Jaji Rabia Hussein Mohamed, amesema watahakikisha wanatoa elimu kwa wapiganaji na màafisa ili waweze kutambua uwepo wake na jinsi ya kuitumia.  .... BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO

mahkama rufaa 5

mahkama rufaa 4

mahkama rufaa 2

mahkama rufaa 1

Kupatikana kwa hati miliki ya umiliki wa maeneo ya Kambi za Kikosi cha Valantia, kutakiwezesha Kikosi hicho kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed, amesema hatua hiyo ya umiliki itaepusha kutokea migogoro isiyo ya lazima ya kugombea ardhi kati ya kikosi hicho na wananchi.

Akitembelea kambi za kikosi cha Valantia Unguja, Mh. Masoud Ali Mohammed amewakumbusha Maafisa na Wapiganaji kusimamia suala la uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa uadilifu.

Akizungumzia juu ya ziara hiyo mkuu wa kikosi cha Valantia, Meja Said Ali Shamhuna, amesema maagizo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha ufanisi unapatikana.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA ZAIDI KW NJIA YA VIDEO..

1 ziara kvz

2 ziara kvz

3 ziara kvz

TAARIFA KWA UMMA

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Msingi wa maamuzi haya unaotokana na ziara nilizozifanya nikiwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Ripoti zilizowasilishwa kwangu na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA), pamoja na vyanzo vyengine vya taarifa.

Tumebaini mambo mengi yakiwemo ubadhirifu wa mali za umma, urasimu, vitendo vyenye harufu ya rushwa na uwajibikaji usioridhisha kwenye maeneo ya Manispaa, Halmashauri na Mabaraza ya Miji pamoja Kandarasi zisizofuata taratibu za kisheria.

Kwa msingi huo ndugu wanahabari na umma tumeamua kuchukua hatua/maamuzi yafuatayo kwa maslahi ya Zanzibar yetu:-

 1. Kumsimamisha kazi na kupisha uchunguzi zaidi Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini na nafasi yake itakaimiwa na mtu mwengine tutakaempatia taarifa kwa mujibu wa sheria
 1. Kumsimamisha kazi na kupisha uchunguzi zaidi Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharibi ‘A’ na nafasi yake itakaimiwa na mtu mwengine tutakaempatia taarifa kwa mujibu wa sheria
 1. Namuagiza Mkuu wa JKU kuivunja Bodi ya Zabuni ya JKU ili kupisha uchunguzi zaidi na hatua za kisheria kuchukuliwa. Aidha, namuagiza Mkuu huyo kuunda Bodi mpya ya Zabuni.
 1. Nawaagiza Wakuu wote wa Idara Maalum za SMZ kufanya uhakiki wa watumishi wote na naagiza kwa mwezi wa Januari 2021 mishahara yote ilipwe kupitia dirishani (cash) badala ya Benki ili kukidhi matakwa ya uhakiki huo.
 2. Namuagiza Mkuu wa JKU kuwaweka pembeni na kupisha uchunguzi zaidi watendaji wa Kitengo cha hesabu, Kitengo cha Manunuzi, Kitengo cha Mipango na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi.
 1. Namuagiza Mkurugenzi atakaekaimu Manispaa ya Mjini kuupitia upya mkataba wa tozo za Magesho (Parking) kati yake na Kampuni ya ECONEX, na kwa vile mkataba huo unaonesha mapungufu mengi, ndani ya wiki mbili zijazo uwe umepitiwa na kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, vyenginevyo naagiza uvunjwe.
 1. Nawaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wote kutathmini upya na kwa uharaka uwezo wa utendaji kazi wa Masheha wote na Kamati zao za Shehia na endapo wakabaini kuna udhaifu katika baadhi ya watendaji hao watengue teuzi zao na kupata watendaji wapya watakaohudumu kwa uadilifu.
 1. Tunaiomba Afisi ya Mwanasheria Mkuu na tutawaandikia rasmi hapo baadae kupitia upya mikataba yote iliyoingiwa na Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ ambayo inaendelea na Kandarasi katika Afisi hii.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Mabaraza ya Manispaa, Mabaraza ya Mijia na Halshauri za Wilaya kuwabadilisha Watendaji wote wanaohudumu katika Vitengo vya Hesabu, Manunuzi na Mapato.
 1. Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kuhakikisha kuwa nyumba ya Kituo cha Afya Uroa iliyobomolewa na mtu aliyepatiwa nyumba hiyo kinyume na utaratibu ahakikshe kuwa wote waliohusika wanafikishwa katika vyombo vya sheria.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri kusimamia vyema na upya suala la ukusanyaji wa kodi zilizopo katika vyanzo vya mapato vilivyo katika maeneo yao na zitozwe kwa mujibu wa sheria.
 1. Nawaagiza Idara Malum za SMZ kuanzia sasa kushiriki katika masuala ya kijamii hasa suala la usafi wa mji wetu kuanzia wiki inayofuata.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri kuongeza nguvu katika eneo la usafi wa mji wetu.

……………………..

MASOUD A. MOHAMMED

WAZIRI WA NCHI - AFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

ZANZIBAR.

Kampuni ya Premium Audit Consulting Limited imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Sekta ya Afya na kutunza mazingira kwa lengo la kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Premium Audit Consulting Limited Bi. ANY IVAN alipokuwa akimkabidhi makontena ya kuhifadhia taka 370 na vitakasa mikono boksi 83 vyenye thamani ya millioni 750 kwa ndugu Khalid Abdallah Omari Naibu Katibu Mkuu Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ huko Afisini kwao Kisauni.

Aidha Mkurugenzi ANY ameahidi kuendeleza ushirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Romania katika Sekta ya Afya ili kuepusha maradhi ya miripuko kwa wananchi pamoja na kuweka safi mazingira ya Mji wa Zanzibar.

Nae Naibu Khalid ameishukuru Serikali ya Romania na kuahidi kuvifanyia kazi vifaa hivyo kwa kuvisambaza katika Manispaa na Mabaraza ya Miji sita (6) ya Unguja na Pemba kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi na kutunza mazingira.

Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 18 - 11 - 2020.

 naibu2  ivan
Ndugu. KHALID ABDALLAH OMAR - Naibu Katibu Mkuu Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Bi. ANY IVAN - Mkurugenzi wa Kampuni ya Premium Audit Consulting Limited
 makabidhiano  madebe 2
Picha ya Makabidhiano Makontena ya kuhifadhia taka (370)

 

Kwa taarifa zaidi tembelea katika kurasa ya "MAKTABA YA VIDEO" kupitia link https://tamisemim.go.tz/index.php/habari/makvideo iliyopo katika tovuti yetu, Au kupitia youtube channel yetu "AR TMIM ZANZIBAR" kupitia https://www.youtube.com/channel/UCxTRE7MzsMY8ORT0dnSMmag

Kushoto  ni  Naibu Katibu Mkuu kutoka Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Nd. KHALID ABDALLAH OMAR na kulia ni Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Idrisa Muslihi Hija. Makabidhiano hayo yaliyofanyika tarehe 23/09/2019. Katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zannzibar. Bofya hapa kupata video..

mkb2

Aliekuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe: Haji Omar Kheri wakiwa pamoja na aliekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh: Riziki Pembe Juma katika kikao cha makabiziano ya Skuli ya Fuoni Mambosasa kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

mkb3

Aliekuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe: Haji Omar Kheri kushoto akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya Skuli ya Msingi Mambosasa, na kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh: Riziki Pembe Juma.

mkb4

Wakitiliana saini katika makabidhiano ya skuli ya msingi ya Mambosasa kushoto ni Naibu Katibu Mkuu kutoka Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd: Khalid Abdallah Omar na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd : Idrisa Muslihi  Hija.

Juu ni picha ya pamoja katika Ufunguzi wa Fisheries Ranger Post....        Bofya hapa kupata video

03mapinduzi56

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Haji Omar Kheir akizindua mradi wa kuimarisha nyumba za kihistoria ya Mwinyi Mkuu iliyopo Wilaya ya Kati Dunga.

02mapinduzi56

Katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Khamis Juma Mwalimu akikata utepe wa jiwe la msingi kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma. Kulia ni Katibu Mkuu OR-TMSMIM Mh. Radhiya Rashid Haroub.

04mapinduzi56

Naibu Katibu Mkuu OR-TMSMIM Mh. Khalid Abdallah Omar akitoa maelezo ya kitaalamu ya Jengo la Skuli ya Pongwe Pwani.

Page 1 of 2

Wasiliana nasi


Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

P.O BOX 4220

Vuga - Zanzibar

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

2550537
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
7821
12178
42595
259685
2550537