Habari na Matukio

Habari na Matukio (10)

Mafunzo ya mfumo wa E-Office kwa Maafisa Tehama, Utumishi na Masjala kwa Taasisi za OR-TMSMIM yaliyofanyika Vuga
09 Sep 2022
masjala 1  masjala 2
 Mafunzo ya mfumo wa E-Office kwa watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ. Mafunzo ya mfumo wa E-Office kwa watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.
masjala 3 masjala 5
 Mafunzo ya mfumo wa E-Office kwa watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ  
Ghafla ya Utiaji Saini kwa Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ kuhusu Ujenzi wa Masoko Mkoa wa Mjini Magharibi
09 Sep 2022
 99 2  99 6
 Utiaji Saini kwa Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ kuhusu ujenzi wa Masoko Mkoa wa Mjini Magharibi.  Utiaji Saini kwa Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ kuhusu ujenzi wa Masoko Mkoa wa Mjini Magharibi.
 99 5  99 4
 Utiaji Saini kwa Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ kuhusu ujenzi wa Masoko Mkoa wa Mjini Magharibi.  
Makabidhiano ya kazi ya ujenzi wa Masoko Mkoa Mjini Magharibi kwa Vikosi vya Idara Maalum za SMZ
08 Sep 2022
 89 1  89 2
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Idrissa Mustafa Kitwana akimkabidhi kazi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar - JKUZ (Col. Makame Abdalla Daima)  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Idrissa Kitwana Mustafa akimkabidhi kazi Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar (Khamis Bakar Khamis)
 89 3  89 4
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh.Idrissa Kitwana Mustafa akimkabidhi kazi Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar - KZU (Rashid Mzee Abdallah)  
Waziri wa OR-TMSMIM Mhe. Masoud akutana na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar ofisini kwake Vuga
05 Sep 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Masoud Ali Mohammed Akizungumza na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad alipokwenda kujitambulisha Ofisini kwake Vuga.

Mhe. Masoud amesema suala la ulinzi wa raia na mali zao ni jambo muhimu ambalo litawaongezea imani wananchi kutoa ushirikano kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Nae Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar amependekeza kuandaliwa kwa mafunzo ya pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Vikosi vya Idara Maalum ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wapiganaji hao. Kamishna Hamad Khamis Hamad amefika Ofisini hapo ujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni

Kwahabari zaidi usiache kutembelea Youtube Channel yetu OR-TMSMIM ZANZIBAR na kusubscribe

 kms1  kms5
 kms4  kms3
Kikao cha ushirikiano kati ya Wajumbe wa jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania na Wajumbe wa Serikali za Mitaa Zanzibar.
02 Sep 2022
 wz1  wz2
 Waziri OR-TMSMIM Mh. Masoud Ali Mohammed, akifungua kikao cha ushirikiano kati ya Wajumbe wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania na Wajumbe wa Serikali za Mitaa Zanzibar Ofisini kwake Vuga.  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania Nd. Murshid Ngeze akizugumza katika kikao cha ushirikiano kati ya Meya na Wakurugenzi wa Manispaa za Zanzibar na Wajumbe wa Serikali za Mitaa Tanzania.
 wz3  wz4
 Waziri OR-TMSMIM Mh. Masoud Ali Mohammed, akifungua kikao cha ushirikiano kati ya Wajumbe wa Jumuiya za Serikali za Mitaa Tanzania na Wajumbe wa Serikali za Mitaa Zanzibar Ofisini kwake Vuga.  
Ziara ya kutembelea kazi za ujenzi katika kambi nne za KVZ
29 Jun 2022
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, amesema usimamizi mzuri katika ujenzi wa makaazi ya askari wa kikosi cha Valantia, utawezesha nyumba hizo kuwa katika kiwango cha ubora.
 
Akitembelea kazi za ujenzi katika kambi nne za KVZ, ameelezea kuridhishwa na Kasi ya ujenzi inavyoendelea Kwa kuwatumia mafundi wa kikosi hicho, Jambo ambalo linaonesha uzalendo na litapunguza gharama za matumizi ya fedha.
Hivyo ameutaka uongozi wa Kikosi hicho kuzidisha ushirikiano na wazabuni ili kuweza kufanikisha vyema miradi hiyo.
 
Nae Mkuu wa Kikosi cha Valantia KVZ, Luteni Kanal Said Ali Shamuhuna, amesema hadi sasa vifaa vya ujenzi vipo vya kutosha na anatarajia ujenzi huo utamalizika kwa wakati uliopangwa na utakuwa na ubora wa kiwango kinachotakiwa.
 
 Ujenzi huo unaoendelea katika kambi ya Muyuni, Kikungwi, Mto wa maji na kambi Mwanyanya, umejumuisha nyumba za kulala askari, nyumba za Wakuu wa zoni pamoja na Ofisi.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 zkvz2  zkvz3
 zkvz4  zkvz5
Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya duniani. 26/06/2022
29 Jun 2022

Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya duniani. 26/06/2022. Kwa upande wa Zanzibar yamefanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge.

 

 mdw2  mdw3
 mdw4  mdw7
 mdw5  mdw6
Mafunzo elekezi kwa Maafisa Manunuzi wa OR-TMSMIM
23 Jun 2022

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Issa Mahfoudh Haji, amesema miradi mingi inayotekelezwa ya ujenzi, imekuwa ikikabiliwa na kasoro za manunuzi. Akifungua mafunzo ya siku mbili Kwa maafisa manunuzi wa Ofisi hiyo, amesema tatizo hilo litapata ufumbuzi Kwa kuwajengea uwezo watendaji waweze kuielewa vyema Sheria ya manunuzi.

Amesema uelewa wa Sheria ya manunuzi na uondoshaji wa Mali za umma, iwe ni chanzo muhimu cha kuleta mabadiliko ya kiutendaji.

Akiwasilisha mada ya Sheria ya manunuzi, Mkufunzi Hafidh Rashid, amesema kuwepo Kwa Sheria hiyo kutaimarisha utawala bora, kulinda haki na wajibu, kutatua migogoro ya ununuzi na na kuishauri Serikali kuhusiana na ununuzi. 3/6/2022 ZANZIBAR.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 mfz  utm7
 utm6  utm5
Mafunzo ya Kujenga Uwezo wa Kuzitambua Kanuni za Utumishi kwa Maafisa wa OR-TMSMIM
23 Jun 2022

Viongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kujenga uwezo wa kuzitambua kanuni za utumishi. Mafunzo hayo yalifanyika siku ya tarehe 22 Juni, 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Mji Magharib “B”

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 utm3  utm1
 utm2  
Kiasi cha milioni mia tatu (300,000,000/=) zakabidhiwa kwa wakulima 135 waliouza zao la miwa kutoka kiwanda cha sukari Mahonda Zanzibar
31 Mar 2021

Wakulima 135 waliouza zao la miwa msimu huu wakabidhiwa kiasi cha 300,000,000/= kutoka Kiwanda cha Sukari Mahonda Zanzibar, ambapo Chuo cha Mafunzo Zanzibar kimepata hundi ya milioni hamsini (50,000,000/=).

Akikabidhi hundi kwa wakulima binafsi pamoja na Jehi la Kujenga Uchumi JKUZ na Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMIM Mhe. Masoud Ali Mohammed amewaomba wananchi kuona umuhimu wa kubadilika na kuzalisha zao la miwa kwani lina tija na soko la uhakika

Aidha amesema uwekezaji wa kiwanda hicho hupeleka kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kuimarisha soko la ndani, hivyo ameagiza kwa Idara Maalum za SMZ kujitathmini na kuangalia uwezekano wa kuyatumia maeneo ya kilimo kwa kuimarisha wakulima wa miwa.

BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.

 1 kiwanda miwa  2 kiwanda miwa
   

Wasiliana nasi


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

2277 Barabara ya Vuga,

S.L.P 4220,

70401 Mjini Magharibi,

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

2872322
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
1164
3078
8997
73438
2872322