Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed, amesema usimamizi mzuri katika ujenzi wa makaazi ya askari wa kikosi cha Valantia, utawezesha nyumba hizo kuwa katika kiwango cha ubora.
Akitembelea kazi za ujenzi katika kambi nne za KVZ, ameelezea kuridhishwa na Kasi ya ujenzi inavyoendelea Kwa kuwatumia mafundi wa kikosi hicho, Jambo ambalo linaonesha uzalendo na litapunguza gharama za matumizi ya fedha.
Hivyo ameutaka uongozi wa Kikosi hicho kuzidisha ushirikiano na wazabuni ili kuweza kufanikisha vyema miradi hiyo.
Nae Mkuu wa Kikosi cha Valantia KVZ, Luteni Kanal Said Ali Shamuhuna, amesema hadi sasa vifaa vya ujenzi vipo vya kutosha na anatarajia ujenzi huo utamalizika kwa wakati uliopangwa na utakuwa na ubora wa kiwango kinachotakiwa.
Ujenzi huo unaoendelea katika kambi ya Muyuni, Kikungwi, Mto wa maji na kambi Mwanyanya, umejumuisha nyumba za kulala askari, nyumba za Wakuu wa zoni pamoja na Ofisi.
BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO.
|
|
|
|