Mahkama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ imetakiwa kusimamia katika kutoa maamuzi bila ya hofu ili kuwatendea haki wapiganaji wanaopeleka malalamiko yao.
Akizungumza na wajumbe wa Mahkama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za mikoa serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed ameitaka Mahkama hiyo kushughulikia rufaa zinazowasilishwa na kuzipatia ufumbuzi.
Aidha ameiomba Mahkama hiyo kuwa na ushirikiano na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum za SMZ ili kurahisisha masuala ya kiutendaji na kupunguza idadi ya kesi.
Mwenyekiti wa Mahkama ya rufaa ya Idara maalum za SMZ Jaji Rabia Hussein Mohamed, amesema watahakikisha wanatoa elimu kwa wapiganaji na màafisa ili waweze kutambua uwepo wake na jinsi ya kuitumia. .... BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA VIDEO