Kupatikana kwa hati miliki ya umiliki wa maeneo ya Kambi za Kikosi cha Valantia, kutakiwezesha Kikosi hicho kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed, amesema hatua hiyo ya umiliki itaepusha kutokea migogoro isiyo ya lazima ya kugombea ardhi kati ya kikosi hicho na wananchi.
Akitembelea kambi za kikosi cha Valantia Unguja, Mh. Masoud Ali Mohammed amewakumbusha Maafisa na Wapiganaji kusimamia suala la uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa uadilifu.
Akizungumzia juu ya ziara hiyo mkuu wa kikosi cha Valantia, Meja Said Ali Shamhuna, amesema maagizo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha ufanisi unapatikana.
BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA ZAIDI KW NJIA YA VIDEO..