Taarifa kwa Vyombo vya Habari
23 Dec 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

TAARIFA KWA UMMA

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Msingi wa maamuzi haya unaotokana na ziara nilizozifanya nikiwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Ripoti zilizowasilishwa kwangu na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA), pamoja na vyanzo vyengine vya taarifa.

Tumebaini mambo mengi yakiwemo ubadhirifu wa mali za umma, urasimu, vitendo vyenye harufu ya rushwa na uwajibikaji usioridhisha kwenye maeneo ya Manispaa, Halmashauri na Mabaraza ya Miji pamoja Kandarasi zisizofuata taratibu za kisheria.

Kwa msingi huo ndugu wanahabari na umma tumeamua kuchukua hatua/maamuzi yafuatayo kwa maslahi ya Zanzibar yetu:-

 1. Kumsimamisha kazi na kupisha uchunguzi zaidi Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini na nafasi yake itakaimiwa na mtu mwengine tutakaempatia taarifa kwa mujibu wa sheria
 1. Kumsimamisha kazi na kupisha uchunguzi zaidi Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharibi ‘A’ na nafasi yake itakaimiwa na mtu mwengine tutakaempatia taarifa kwa mujibu wa sheria
 1. Namuagiza Mkuu wa JKU kuivunja Bodi ya Zabuni ya JKU ili kupisha uchunguzi zaidi na hatua za kisheria kuchukuliwa. Aidha, namuagiza Mkuu huyo kuunda Bodi mpya ya Zabuni.
 1. Nawaagiza Wakuu wote wa Idara Maalum za SMZ kufanya uhakiki wa watumishi wote na naagiza kwa mwezi wa Januari 2021 mishahara yote ilipwe kupitia dirishani (cash) badala ya Benki ili kukidhi matakwa ya uhakiki huo.
 2. Namuagiza Mkuu wa JKU kuwaweka pembeni na kupisha uchunguzi zaidi watendaji wa Kitengo cha hesabu, Kitengo cha Manunuzi, Kitengo cha Mipango na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi.
 1. Namuagiza Mkurugenzi atakaekaimu Manispaa ya Mjini kuupitia upya mkataba wa tozo za Magesho (Parking) kati yake na Kampuni ya ECONEX, na kwa vile mkataba huo unaonesha mapungufu mengi, ndani ya wiki mbili zijazo uwe umepitiwa na kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, vyenginevyo naagiza uvunjwe.
 1. Nawaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wote kutathmini upya na kwa uharaka uwezo wa utendaji kazi wa Masheha wote na Kamati zao za Shehia na endapo wakabaini kuna udhaifu katika baadhi ya watendaji hao watengue teuzi zao na kupata watendaji wapya watakaohudumu kwa uadilifu.
 1. Tunaiomba Afisi ya Mwanasheria Mkuu na tutawaandikia rasmi hapo baadae kupitia upya mikataba yote iliyoingiwa na Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ ambayo inaendelea na Kandarasi katika Afisi hii.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Mabaraza ya Manispaa, Mabaraza ya Mijia na Halshauri za Wilaya kuwabadilisha Watendaji wote wanaohudumu katika Vitengo vya Hesabu, Manunuzi na Mapato.
 1. Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kuhakikisha kuwa nyumba ya Kituo cha Afya Uroa iliyobomolewa na mtu aliyepatiwa nyumba hiyo kinyume na utaratibu ahakikshe kuwa wote waliohusika wanafikishwa katika vyombo vya sheria.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri kusimamia vyema na upya suala la ukusanyaji wa kodi zilizopo katika vyanzo vya mapato vilivyo katika maeneo yao na zitozwe kwa mujibu wa sheria.
 1. Nawaagiza Idara Malum za SMZ kuanzia sasa kushiriki katika masuala ya kijamii hasa suala la usafi wa mji wetu kuanzia wiki inayofuata.
 1. Nawaagiza Wakurugenzi wa Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri kuongeza nguvu katika eneo la usafi wa mji wetu.

……………………..

MASOUD A. MOHAMMED

WAZIRI WA NCHI - AFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

ZANZIBAR.

Last modified on Monday, 28 December 2020 05:48

Wasiliana nasi


Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

P.O BOX 4220

Vuga - Zanzibar

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

860514
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
835
6859
31351
119687
860514