Bonaza la kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto lililoandaliwa na Baraza la Manispaa Mjini - Zanzibar
29 Nov 2019

Bonaza la kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto lililoandaliwa na Baraza la Manispaa Mjini - Zanzibar

Baraza la Manispaa Mjini liliandaa bonaza la kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto na kulikua na upimaji wa afya (HIV) bure. Mgeni rasmi katika Bonanza hilo ambalo Skuli mbalimbali zilishiriki alikuwa ni Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Ndugu. Said Juma Ahmada.

Katika bonanza hilo ushindi ulikwenda kwa Skuli ya Muungano na walipata zawadi ya tsh. laki mbili (200,000/=) na seti ya jezi, mpira na kombe. Aidha mshindi wa pili alipata zawadi na tsh. laki moja (100,000/=), jezi pamoja na mpira. Bonanza hilo lilifanyika katika viwanja vya michezo vya Mao Tse Tung Mjini Zanzibar.

0020

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Ndugu. Said Juma Ahmada akipima (HIV) katika bonaza la kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto lililoandaliwa na Baraza la Manispaa Mjini.

0018

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Ndugu. Said Juma Ahmada akikabidhi zawadi kwa washindi wa bonaza la kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto lililoandaliwa na Baraza la Manispaa Mjini.

0019

Last modified on Friday, 29 November 2019 07:06

Wasiliana Nasi


Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

P.O BOX 4220

Vuga - Zanzibar

Tel: +255242230034

Fax: +255242230034

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Waliotembelea Tovuti

178681
Today
Yesterday
This Week
This Month
All days
1433
944
2963
11547
178681